Psalms 139

Mungu Asiyeweza Kukwepwa

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)


1 aEe Bwana, umenichunguza
na kunijua.

2 bUnajua ninapoketi na ninapoinuka;
unatambua mawazo yangu tokea mbali.

3 cUnafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu;
unaelewa njia zangu zote.

4 dKabla neno halijafika katika ulimi wangu,
wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana.


5 eUmenizunguka nyuma na mbele;
umeweka mkono wako juu yangu.

6 fMaarifa haya ni ya ajabu mno kwangu,
ni ya juu sana kwangu kuyafikia.


7 gNiende wapi nijiepushe na Roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?

8 hKama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko;
nikifanya vilindi
Vilindi ina maana ya Kuzimu, ambayo ni Sheol kwa Kiebrania.
kuwa kitanda changu,
wewe uko huko.

9 Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko,
kama nikikaa pande za mbali za bahari,

10 jhata huko mkono wako utaniongoza,
mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti.


11 Kama nikisema, “Hakika giza litanificha
na nuru inayonizunguka iwe usiku,”

12 khata giza halitakuwa giza kwako,
usiku utang’aa kama mchana,
kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.


13 lKwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;
uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

14 Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa
kwa namna ya ajabu na ya kutisha;
kazi zako ni za ajabu,
ninajua hayo kikamilifu.

15 mUmbile langu halikufichika kwako,
nilipoumbwa mahali pa siri.
Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

16 nmacho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.
Siku zangu zote ulizonipangia
ziliandikwa katika kitabu chako
kabla haijakuwepo hata moja.


17 oTazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu!
Jinsi jumla yake ilivyo kubwa!

18 pKama ningezihesabu,
zingekuwa nyingi kuliko mchanga.
Niamkapo,
bado niko pamoja nawe.


19 qLaiti ungewachinja waovu, Ee Mungu!
Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu!

20 rWanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya,
adui zako wanatumia vibaya jina lako.

21 sEe Bwana, je, nisiwachukie wanaokuchukia?
Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako?

22 tSina kitu zaidi ya chuki dhidi yao,
ninawahesabu ni adui zangu.


23 uEe Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu,
nijaribu na ujue mawazo yangu.

24 vUone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu,
uniongoze katika njia ya milele.
Copyright information for SwhKC